Fungua Akaunti ya OSF (Create an OSF Account)

Hii Makala imeidhinishwa Chini ya leseni CC0 Kwa matumizi ya Umma wote

OSF ni bure kutumia. Ukiwa na akaunti ya ORCiD au una akaunti toka  mojawapo ya Taasisi ambazo ni Washirika wetu, unaweza kufungua akaunti yako ya OSF kwa kutumia njia hizi. ORCiD au akaunti toka taasisi yako na itaunganishwa moja kwa moja na akaunti yako ya OSF.

Nenda kwa OSF, kisha bonyeza kitufe cha kujisajili katika sehemu ya juu ya kulia ya ukurasa wa mwanzo wa OSF.

OSF Homepage

Fungua akaunti yako kwa kutumia ORCiD au taarifa za akaunti yako toka taasisi yako .

Au, ingiza jina lako, barua pepe, na nywila katika sehemu husika.

Create Your Account

Soma Masharti ya Matumizi (Kiingereza) na Sera ya  faragha (Kiingereza), kisha chagua na uweke alama katika kisanduku karibu na "Nimesoma na kukubali."

Chagua na uweke alama katika  kisanduku karibu na "Mimi si roboti," kisha ubofye kitufe cha Kujisajili.

Captcha

Utapokea barua pepe ya uthibitisho kutoka kwa OSF kwenye anwani ya barua pepe uliyotumia kufungua akaunti yako.

Bofya hicho kiungo katika barua pepe ili kuthibitisha anwani yako ya barua pepe.

Akaunti yako ya OSF itakuwa sasa imefunguliwa.

Hii Makala imeidhinishwa Chini ya leseni CC0 Kwa matumizi ya Umma wote.

Did this answer your question? Thanks for the feedback There was a problem submitting your feedback. Please try again later.