Hifadhi ya Mradi na Upakiaji wa Faili (Project Storage and File Upload)

cc-zero.png   Hii Makala imeidhinishwa Chini ya leseni CC0 Kwa matumizi ya Umma wote

Hifadhi ya mradi 

OSF inaweka kikomo uwezo wa miradi ya kibinafsi na vipengee vinavyotumia Hifadhi ya OSF hadi GB 5 na miradi ya umma na vipengele vyake hadi GB 50 na kuwashauri watumiaji kujumuisha Viongezo.(Kiingereza) kwenye miradi yao ili visaidie katika usimamizi wa hifadhi ya miradi kadri inapowezekana. Kwa maelezo zaidi tafadhali angalia miongozo yetu ya msaada juu ya uhifadhi wa mradi hapa chini;

Kila mradi na kipengele inaweza kuwa na seti yake ya faili, kukuruhusu kupanga faili zako katika vikundi vya kategoria au madaraja, kama seti za data au masomo. Kila faili ina URL ya kipekee, inayodumu ili iweze kunukuliwa au kurejea kwa kuunganishwa kwa kila moja. Faili za kibinafsi zilizopakiwa kwenye Hifadhi ya OSF lazima ziwe na GB 5 au chini. Faili kubwa zaidi zinaweza kuhifadhiwa kwenye Kiongezi (Kiingereza).

Upakiaji wa Faili

Anza kwa kubofya kichupo cha faili kilicho juu ya ukurasa wa mradi wako: 

Ukurasa mpya wa "Faili" utaonekana. 

Chagua kwa kubofyamtoa huduma wa hifadhi (k.m Hifadhi ya OSF, Dropbox, Hifadhi ya Google, n.k.) kwenye upau wa vidhibiti kwenye safu wima ya kushoto. Mtoa huduma wa hifadhi aliyechaguliwa kwa sasa atanaonekana  kwa  herufi nzito:

Bofya kitufe cha kijani kibichi(+) 

Bofya "Pakia faili" 

Chagua ”faili” kutoka kwa kisanduku cha mazungumzo kitakacho onekana.

Buruta na uangushe

Au, buruta na udondoshe faili kutoka kwa kompyuta yako hadi kwa eneo la awali la “mtoa huduma wa hifadhi”.

Faili ulizochagua zitaongezwa kwenye mradi wako.


Boakye, E., Abdullah, B., Aziz, K., Kevin, B., Kiage, B., Lisso, F., … Wesonga, R. M. (2023, May 9). Phase 1: Getting Started Help Guides (Swahili). https://doi.org/10.17605/OSF.IO/RKTHV

Did this answer your question? Thanks for the feedback There was a problem submitting your feedback. Please try again later.

Still need help? Contact Us Contact Us