Ingia kwa OSF (Sign in to OSF)

cc-zero.png

  Hii Makala imeidhinishwa Chini ya leseni CC0 Kwa matumizi ya Umma wote. 

Unaweza kuingia kwa OSF kwa kutumia jina i na nywilai ulilotumia kufungua akaunti au taarifa za akaunti yako toka  taasisi yako au taarfia toka ORCiD akaunti. Unaweza kuvinjari na kusoma ukurasa wa  OSF bila kuingia kwa kutumia akaunti; hata hivyo,  ili kutumia bidhaa za OSF na kudhibiti kazi yako utahitaji kuingia kwa kutumia akaunti yako ya OSF.

  • Nenda kwa Ukurasa wa OSF"Ingia"
  • Ingia  Kwa kutumia  Barua Pepe Yako na Nywila ya OSF
  • Ingia Kupitia ORCID
  • Ingia Kupitia Akaunti binafsi toka taasisi yako
  • Akaunti Iliyozimwa Au Iliyoripotiwa kuwa ya kutiliwa shaka

Nenda kwenye ukurasa wa OSF wa "ingia"

Bofya kitufe cha ingia upande wa juu kulia wa Ukurasa wa mwanzo wa OSF.

Ukurasa wa OSF"Jisajili"   utaonekana.

Ingia kwa kutumia barua pepe na nywila yako

Ingiza barua pepe na nywila uliyotumia kufungua akaunti yako ya OSF.

Kisha, bofya kitufe cha INGIA.

Sasa utakuwa umeingia kwenye akaunti yako ya OSF na kupelekwa kwenye Dashibodi yako.

Ingia kupitia ORCiD  

Tafadhali fahamu hali zifuatazo:

  • Unapoingia kwenye OSF kwa kutumia taarifa za akaunti ya  ORCiD na huna akaunti ya OSF, moja kwa moja akaunti mpya ya OSF itafunguliwa  kwa kutumia taarifa za  akaunti yako ya ORCiD.
  • Ukiwa na akaunti ya OSF, na unatumia barua pepe ile ile kwa akaunti zako zote mbili za OSF na ORCiD, unaweza kuingia kwenye OSF kwa kutumia utambulisho wa  ORCiD na akaunti ya pili ya OSF haitafunguliwa. Katika hali hii, unapoingia kwenye OSF kwa kutumia taarifa za akaunti ya  ORCiD, taarifa za akaunti yako ya  ORCiD zitaongezwa moja kwa moja  kwenye akaunti yako ya OSF.
  • Ikiwa barua pepe ya  kwenye akaunti yako ya OSF ni tofauti na barua pepe ya kwenye akaunti ya ORCiD, basi kuingia kwenye OSF kupitia ORCiD, moja kwa moja kutakufungulia  akaunti ya pili ya OSF. Ukijipata katika hali hii, tafadhali angalia mwongozo wetu Unganisha Akaunti Zako (Kiingereza) kwa maelekezo.

Bofya kitufe cha Ingia kwa kutumia ORCID ili kuingia kwenye OSF kwa kutumia utambulisho wa ORCiD.  

Utapelekwa kwenye ukurasa wa "OAuth" wa ORCiD.

Bofya kitufe cha Idhinisha ili kutoa idhini ya kufikia OSF kwa kutumia taarifa zako za akaunti  ya ORCiD.

ORCID Sign In Page

Sasa utakuwa umeingia kwenye akaunti yako ya OSF na kupelekwa kwenye Dashibodi yako.

Ingia kupitia utambulisho toka taasisi yako

Ikiwa taasisi yako ni mshirika wa OSF (yaani wana Ukurasa wa Kutua wa Kitaasisi), unaweza kuingia kwenye OSF kwa kutumia taarifa za akaunti yako toka taasisi yako. Ikiwa hapo awali ulitumia utambulisho waa kitaasisi kuingia  lakini sasa huwezi kupata taasisi yako kwenye orodha kunjuzi, Tembelea Mwongozo Huu (Kiingereza) kwa hatua za kufuata kuendelea kufikia na kutumia akaunti yako ya OSF.

Bofya Ingia kupitia kitufe cha taasisi.

Chagua taasisi yako kutoka kwenye menyu kunjuzi ya Chagua taasisi yako, kisha bofya Ingia.

itakupeleka kwenye ukurasa wa ”Ingia” wa taasisi yako. Weka taarifa binafsi kutoka taasisi yako, na kisha itakurejesha kwenye ukurasa wa  OSF.

Ikiwa hukuwa na akaunti ya OSF hapo awali, utaombwa kusoma na kukubaliana na Masharti ya Matumizi (Kiingereza) na Sera ya Faragha (Kiingereza).

Kisha bofya kitufe cha Endelea.

Utaingia kwenye akaunti yako ya OSF na kupelekwa kwenye Dashibodi yako.

Kutumia njia zaidi ya moja (njia mbadala) za Kuingia katika akaounti yako.

Kuwa na njia zaidi ya moja ya kuingia katika akaunti  kutahakikisha kwamba unadumisha ufikiaji wa akaunti yako hata kama anwani yako ya barua pepe, taasisi, au maelezo mengine yatabadilika. Unaweza kutumia chaguo zote hapo juu (njia zaidi ya moja) kwenye akaunti moja. Ukigundua kuwa una akaunti nyingi za OSF, unaweza kuziunganisha. Tazama Zaidi Kuhusu Kuunganisha Akaunti Hapa (Kiingereza).

Akaunti Iliyozimwa au Iliyoripotiwa kuwa ya kutiliwa shaka

Ikiwa una akaunti au nyenzo ambayo imetahadharishwa kwa uwongo kuwa ni ya kutiliwa shaka au imezimwa tafadhali ripoti taarifa yako kwetu kwa kujaza "Akaunti Imezimwa Au Imetahadharishwa Kwa Uongo Kama ya kutiliwa shaka". Usaidizi wa OSF hukagua ripoti hizi kwa msingi wa kesi kwa kesi. 

Did this answer your question? Thanks for the feedback There was a problem submitting your feedback. Please try again later.