Unda Mradi (Create a Project)
Hii Makala imeidhinishwa Chini ya leseni CC0 Kwa matumizi ya Umma wote.
Miradi ya OSF ndiyo aina kubwa zaidi ya uainishaji wa kivigezo ambao OSF inasaidia. Mradi unaweza kuwa jaribio, kikundi cha maabara, au karatasi—chochote ambacho kina washiriki na faili zinazochangia au maandishi/picha za maelezo.
- Unda Mradi Mpya
- Weka Jina la Mradi
- Ongeza Uhusishi wa Kitaasisi (Si lazima)
- Chagua Eneo la Hifadhi
- Weka Maelezo
- Kamilisha Mradi Wako
Unda mradi mpya
Ingia katika OSF, kisha bofya kitufe cha Unda mradi mpya kwenye dashibodi yako.
Modali ya "Unda mradi mpya" itaonekana.
2. Weka Jina
Weka Jina la Mradi wako kwenye Sehemu ya "Jina".
3. Ongeza ushirika wa kitaasisi (si lazima)
Ikiwa umeingia kwenye OSF kupitia tovuti ya kitaasisi, miradi mipya iliyoundwa itahusishwa na taasisi hiyo kwa chaguo-msingi.
Taasisi zinazohusishwa na akaunti yako ya OSF zitachaguliwa kwa chaguomsingi. Ondoataasisi yako kwenye chaguo-msingi ili kuunda mradi wako bila uhusisho wa taasisi yako.
4. Chagua eneo la kuhifadhi
Kisha, bofya ndani ya menyu ya "Mahali pa kuhifadhi", kisha uchague eneo kutoka kwenye orodha (eneo lako la kimataifa litawekwa kwa chaguo-msingi):
- Marekani
- Kanada - Montréal
- Ujerumani - Frankfurt
Weka maelezo au chagua mradi kutumia kama kiolezo(si lazima)
Bofya kitufe cha Zaidi, na sehemu ya orodha kunjuzi itaonekana.
Ingiza muhtasari wa mradi wako kwenye sehemu ya "Maelezo".
Ili kupanga mradi wako mpya kulingana na mojawapo ya miradi yako iliyopo, chagua mradi kutoka kwenye menyu (muundo pekee ndio utakaorudufiwa na si maudhui).
Kamilisha mradi wako
Kisha, bofya kitufe cha Unda.
Mradi wako utaundwa.
Bofya kitufe cha Nenda kwa mradi mpya katika modali ili kuelekeza kwenye ukurasa wako wa "Muhtasari wa Mradi".
Ukurasa wa "Muhtasari wa Mradi" ndio mwonekano mkuu wa mradi wako. Kuanzia hapa unaweza kusoma maelezo ya mradi wako, kufikia Wiki (Kiingereza), Pakia Faili, Ongeza Lebo (Kiingereza), na zaidi.
Boakye, E., Abdullah, B., Aziz, K., Kevin, B., Kiage, B., Lisso, F., … Wesonga, R. M. (2023, May 9). Phase 1: Getting Started Help Guides (Swahili). https://doi.org/10.17605/OSF.IO/RKTHV