Hariri Rasimu Yako ya Usajili (Edit Your Draft Registration)
Hii Makala imeidhinishwa Chini ya leseni CC0 Kwa matumizi ya Umma wote.
Mwongozo utakupitisha kwenye mtiririko mkuu wa kazi ili uweze kuhariri rasimu yako ya usajili kwa haraka na mafanikio.
Mada
- Kuupata rasimu yako ya Usajili
- Muundo wa Kiolezo cha Usajili wa Utafiti
- Kusajili Metadata
- Kuongeza, Kuhariri, na Kuondoa Wachangiaji
- Ongeza Mchangiaji
- Ondoa Mchangiaji.
- Uhifadhi
Kuupata Usajili Wako wa Rasimu
Jinsi ya kuupata usajili wako wa rasimu inategemea kama ulianza usajili kutoka mwanzo au usajili kulingana na mradi/kipengele.Njia zote mbili zimejumuishwa hapa chini.
Usajili tupu
Barua pepe inatumwa wakati wowote usajili unapoundwa au mchangiaji anapoongezwa. Hii barua pepe inajumuisha kiungo cha usajili wa rasimu. Bofya kiungo hiki kufungua rasimu ya usajili ili kuendelea na uhariri wako.
Imeanza kutoka kwa mradi/kipengele
Kuna njia mbili za kuupata usajili unaotegemea mradi. Katika njia ya kwanza, barua pepe inatumwa wakati wowote usajili unapoundwa au wakati mchangiaji anapoongezwa. Hii barua pepe inajumuisha kiungo cha usajili wa rasimu. Bofya kiungo hiki kufungua rasimu ya usajili ili kuendelea na uhariri wako.
Njia ya pili ni kufungua mradi wa usajili husika, na kubofya "Usajili" kwenye upau wa urambazaji.
Bofya kichupo cha "Usajili wa rasimu".
Bofya aidha kichwa (1) au kitufe cha "Badilisha" (2) kwenye rasimu ya usajili unaotaka kufungua.
Muundo wa Kiolezo cha Usajili wa Utafiti
Kila kiolezo cha usajili wa utafiti kimeundwa kwa njia tofauti, kila kikiwa na sehemu na maswali yake. Sehemu zimeorodheshwa kwenye paneli ya kushoto. Unaweza kuvinjari sehemu tofauti katika kiolezo cha usajili wa utafiti kwa kutumia kidirisha cha kushoto (1) au kubonyeza vitufe vya "Inayofuata" na Nyuma (2).
Metadata ya Usajili
Sehemu za kwanza kwenye kila kiolezo zitakuomba uweke metadata msingi (Kichwa, Maelezo, n.k.) kuhusu data na utafiti wako. Metadata hii inatumika kuongeza upatikanaji wa usajili wako.
Kumbuka: Metadata hii haitasawazishwa ikiwa umejiandikisha kutoka kwa mradi.
Kuongeza, Kuhariri na Kuondoa Wachangiaji
Unaweza kukagua wachangiaji wako moja kwa moja kwenye usajili wako kwa kutumia wijeti ya Wachangiaji. Wijeti ina vipengele 6 muhimu:
- Jina la mchangiaji anayehusishwa na usajili.
- Kiwango cha ruhusa cha mchangiaji. Bofya menyu kunjuzi na uchague kiwango kinachofaa cha ruhusa. Unaweza kusoma zaidi kuhusu viwango vya ruhusa [hapa <link to guide>].
- Iwapo mchangiaji atajumuishwa katika nukuu ya biblia inapowasilishwa. Wachangiaji walio na alama ya tiki ya samawati wamejumuishwa kwenye dondoo.
- Taarifa za ajira na elimu ya mchangiaji, iwapo zitatolewa. Bofya kishale cha chini ili kufikia maelezo haya.
- Ondoa mchangiaji kwenye usajili. (Soma Zaidi (Kiingereza))
- Ongeza mchangiaji kwenye usajili. (Soma Zaidi (Kiingereza))
Ongeza Mchangiaji
Bonyeza duara la buluu na alama ya kuongeza.
Wijeti ya "Ongeza Mchangiaji" itafunguliwa.
Ili kuongeza mchangiaji ambaye ana akaunti ya OSF, bofya ndani ya sehemu ya utafutaji. Andika jina la mchangiaji, GUID, au Kitambulisho cha ORCID, kisha ubofye "Tafuta".
Orodha ya wachangiaji waliosajiliwa wa OSF itaonekana. Weka mipangilio ya ruhusa (1) na dondoo (2) kwa mchangiaji anayefaa. Baada ya kuweka, bofya ishara ya kijani kibichi (3) ili kuziongeza kwenye usajili.
Ikiongezwa, arifa ya mafanikio itajazwa kwenye skrini ya juu kulia (1), ishara ya kijani kibichi itakuwa tiki (2), na zitaorodheshwa kwenye kidirisha cha "Wachangiaji Sasa" (3). Mchangiaji aliyeongezwa atapokea barua pepe kuwaarifu kuwa wameongezwa na kiungo cha usajili wa rasimu.
Thibitisha na wachangiaji wako kwamba walifanikiwa kuongezwa. Wachangiaji kadhaa wanaweza kuwa na majina sawa na OSF haishiriki barua pepe kwa sababu za faragha. Muhimu: Wachangiaji hawawezi kuhaririwa baada ya usajili kuwasilishwa.
Ondoa Mchangiaji
Chagua "X" nyekundu katika safu mlalo sawa na mchangiaji atakayeondolewa.
Kumbuka: Angalau mchangiaji mmoja wa Msimamizi lazima ahusishwe na rasimu ya usajili.
Dirisha la uthibitisho litaonekana. Bonyeza "Ondoa mchangiaji".
Arifa ya kijani ya mafanikio itaonekana na mchangiaji ataondolewa kwenye orodha ya "Wachangiaji".
Kuhifadhi
rasimu yako huhifadhiwa kiotomatiki ili wewe na/au washirika wako mrudi baadaye. Kiolezo huhifadhi kiotomatiki kila baada ya sekunde chache masasisho yanapofanywa. Unaweza kuondoka kwenye kiolezo na kurudi kwenye rasimu wakati wowote.
Soma jinsi ya Kuwasilisha Rasimu ya Usajili
Boakye, E., Abdullah, B., Aziz, K., Kevin, B., Kiage, B., Lisso, F., … Wesonga, R. M. (2023, May 9). Phase 1: Getting Started Help Guides (Swahili). https://doi.org/10.17605/OSF.IO/RKTHV