uanzisha Usajili mpya (Start a Registration)
Kuna njia mbili za kuanzisha usajili mpya kukuwezesha kutumia jukwaa la OSF:
- Kuanza kutoka mwanzo, kwa njia hii utajaza maelezo na kuambatisha faili unapounda mpango wako wa utafiti.
- Kuanza kutoka kwa mradi au kipengele cha OSF uliopo/kiliopo tayari, kwa njia hii utaanzisha usajili kwa kuvuta metadata na faili kutoka kwa mradi uliopo.
Kwa njia zote mbili, usajili mpya utakuwa na mradi uliounganishwa wa OSF kwa ajili ya kuendeleza mzunguko wa mchakato wa utafiti, ambapo utaweza kuonesha na kushirikisha kazi yako kwa umma.
Mwongozo huu utakuelekeza na kukuwezesha kutumia njia zote mbili za kuwasilisha Usajili wako kwenye jukwaa la OSF. Iwapo ungependelea kuwasilisha kwa sajili yenye chapa inayopangishwa kwenye miundombinu ya OSF, soma mwongozo wetu " Wasilisha kwa Masjala Inayoendeshwa na Jumuiya" (Kiingereza).
Kumbuka: Iwapo unapanga kuwasilisha usajili wako kwa ukaguzi wa wanazuoni bila ya wewe kufahamika, hakikisha kuwa hakuna taarifa ya kukutambua iliyojumuishwa katika metadata yoyote au hati au faili zilizoambataniishwa unapowasilisha usajili wako.
Baada ya kuwasilisha, unaweza Kuunda Kiungo cha Kutazama Pekee (Kiingereza) ili kuficha utambulisho wako na kushirikisha wasilisho lako kwa ukaguzi kutoka kwa wanazuoni. Kiunganishi cha kutazama pekee kisicho onesha utambulisho wako kita ondoa jina lako kwenye ukurasa wa "Muhtasari wa Usajili" na sehemu ya "Waandishi wa Shiriki" ya metadata ya usajili.
Ukishawasilisha usajili, hutaweza kuuhariri au kuufanyia mabadiliko baadaye.
Mada
Anza Usajili Kutoka Mwanzo
Anza Usajili Kutoka Kwa kipengele au Mradi Uliopo tayari
Anza Usajili kutoka Mwanzo
uanza upya, anza kwa kubofya "Ongeza Mpya" katika upau wa kusogeza kutoka ukurasa wa nyumbani wa Usajili wa OSF: https://osf.io/registries?view_only= .
Bofya menyu kunjuzi iliyo karibu na "Nyumbani OSF", kisha ubofye "Rejesta za OSF". Ukurasa wa kutua wa Usajili wa OSF utaonekana.
Ukurasa wa "Ongeza Usajili Mpya" utaonekana.
Bofya "Hapana" kwa "Hatua ya 1: Je, una maudhui ya usajili katika mradi uliopo wa OSF?", ikionyesha kuwa huna mradi au kipengele cha OSF kilichopo tayari ili kutumika kuunda fomu mpya ya usajili.
Chagua kiolezo cha usajili ambacho kinafaa zaidi mradi wako wa utafiti. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu fomu tofauti za usajili zinazopatikana kwenye OSF kwenye mwongozo “ Elewa Fomu za Usajili”. Ikiwa fomu hizi haziambatani na mradi wako wa utafiti, tembelea wiki ya mradi wetu wa “Violezo vya Fomu za Usajili za OSF''. Sehemu ya “Haipatikani kwenye OSF '' inajumuisha maelezo zaidi kuhusu violezo kadhaa vya usajili ambavyo vinakuja hivi karibuni au vinavyopatikana kwenye mifumo mingine.
Iwapo unahitaji usaidizi zaidi katika kuchagua kiolezo kinachofaa cha usajili kwa ajili ya utafiti wako, tafadhali wasiliana nasi kwa njia ya baruapepe: support@osf.io .
Bofya "Unda rasimu", na utapelekwa kwenye kiolezo cha usajili wa rasimu. Sasa, unaweza kuanza kujaza metadata ya usajili na kutoa majibu kwa kiolezo cha usajili ulichochagua.
Barua pepe iliyo na kiungo cha rasimu hii ya usajili itatumwa kwa anwani yako ya barua pepe iliyounganishwa na OSF. Muhimu: Hifadhi kiungo hiki kwa ufikiaji wa baadaye wa rasimu ya usajili wako.
- Jifunze jinsi ya hariri rasimu ya usajili.
- Jifunze jinsi ya kuwasilisha rasimu yako.
Anza Usajili kutoka kwa Mradi au Kipengele kilichopo
Kuna njia 2 zinazofaa za kuanzisha usajili mpya kutoka kwa kipengele au mradi uliopo wa OSF.
- Kutoka kwa Sajili za OSF Kitufe cha "Ongeza Mpya"
- Kutoka kwa Mradi au Kichupo cha "Usajili" cha Kipengele
Kutoka kwa Sajili za OSF kitufe cha "Ongeza Mpya"
Bofya menyu kunjuzi karibu na "OSF nyumbani", kisha ubofye "Rejesta za OSF". Ukurasa wa kutua wa Usajili wa OSF utaonekana.
Bofya "Ongeza Mpya" kwenye upau wa kusogeza.
Ukurasa wa "Ongeza Usajili Mpya" utaonekana.
Bofya "Ndiyo" kwa "Hatua ya 1: Je, una maudhui ya usajili katika mradi uliopo wa OSF?", ikionyesha kuwa una mradi au kipengele cha OSF cha kuunda usajili mpya kutoka.
Orodha kunjuzi ya miradi na vipengele vyako vitaonekana.
Chagua mradi au sehemu ambayo ungependa kuunda fomu ya usajili. Orodha hii itaonyesha miradi au vipengee ambavyo una ruhusa za msimamizi.
Bonyeza "Unda rasimu".
Utapelekwa kwenye kwenye rasimu ya mfano (kiolezo) ya usajili. Hapo, unaweza kuanza kujaza metadata ya usajili na kutoa majibu kwa kiolezo cha usajili ulichochagua.
Barua pepe iliyo na kiungo cha rasimu hii ya usajili itatumwa kwa anuwani yako ya barua pepe iliyounganishwa na OSF. Unaweza kutumia kiungo hiki au uende kwa mradi uliosajiliwa ili kurudi kwenye rasimu ya usajili wako. Soma "Kufikia Usajili Wako wa Rasimu(Kiingereza)" ili kujifunza zaidi.
Jifunze jinsi ya Kuhariri Rasimu ya Usajili.
Jifunze jinsi ya Wasilisha Rasimu ya Usajili.
Kutoka sehemu ya usajili wa mradi Nenda hadi kwenye "Dashibodi" yako.
Tafuta mradi ambao una maudhui unayotaka kusajili. Kuna njia kadhaa za kutafuta miradi:
- Tafuta kwa jina la mradi.
- Bofya "Miradi Yangu" na utafute kupitia ukurasa wako wa "Miradi Yangu". Unaweza kusoma zaidi juu ya kusimamia, kupanga, na kutafuta miradi katika nakala yetu "Dhibiti Miradi Yako (Kiingereza)".
Fungua kichupo cha "Usajili" kwenye mradi au sehemu unayotaka kujumuisha katika usajili. Fuata hatua ndogo hapa chini kwa maelezo.
Ikiwa unataka kusajili mradi
Bofya "Usajili" kwenye kidirisha kidogo cha kusogeza. Hii itakuwezesha kuunda usajili wa mradi mzima, pamoja na vipengele vingine unavyotaka kujumuisha. Baadaye katika mchakato unaweza kuchagua ni vipengele vipi vya kujumuisha katika usajili, au chagua vyote.
Ikiwa unataka kusajili sehemu ya mradi
Bofya ili kufungua sehemu unayotaka kusajili. Hii itafungua ukurasa wa hiyo sehemu.
Bofya "Usajili". Hii itakuruhusu kusajili maudhui ya sehemu hii pekee na vipengele vidogo vipatikanavyo ndani ya hii sehemu. Baadaye katika mchakato unaweza kuchagua ni vipengele gani vidogo vya kujumuisha katika usajili.
Bofya kitufe kilichoandikwa "Usajili mpya", na dirisha litaonekana lenye violezo tofauti vya usajili wa utafiti.
Chagua kiolezo cha usajili wa utafiti kutoka kwenye orodha, kisha ubofye kitufe kilichoandikwa "Unda rasimu". Kiolezo kilichochaguliwa kitaonekana.
Angalia makala yetu " Hariri Rasimu ya Usajili" ili kujifunza jinsi ya kuhariri usajili.
Boakye, E., Abdullah, B., Aziz, K., Kevin, B., Kiage, B., Lisso, F., … Wesonga, R. M. (2023, May 9). Phase 1: Getting Started Help Guides (Swahili). https://doi.org/10.17605/OSF.IO/RKTHV