Kuanza kutumia OSF (Getting started on the OSF)

Karibu!

Je ni Mara ya kwanza kutumia Mfumo wa Sayansi Huria (OSF)? Umechanganyikiwa kuhusu wapi pa kuanzia? Angalia mwongozo wa "Mara ya kwanza kutumia OSF" hapa chini! 

OSF ni mradi wa programu huria wa chanzo huria ambao huwezesha ushirikiano wazi katika utafiti wa sayansi. Kama zana ya ushirikiano, OSF husaidia timu za watafiti kufanya kazi kwenye miradi kwa faragha au kufanya mradi mzima  kufikia umma ili kuwezesha usambazaji mpana. Kama mfumo wa mtiririko wa kazi, OSF huwezesha miunganisho ya data, chapa ya awali ya makala, na usimamizi wa data na upangaji wa tafiti ambao watafiti tayari wanatumia, kurahisisha mchakato wa utafiti na kuongeza ufanisi. Chapisha kazi yako, omba maoni na utagi mada za kitafiti ambazo ungependa wengine wazione , watoe maoni yao na washirikiane nawe. 

Mara ya kwanza kutumia OSF

  1. Fungua Akaunti ya OSF, Ingia kwa OSF   
    1. Anza kwa kutengeneza akaunti yako ya kibinafsi ya OSF. Akaunti za watumiaji hukuwezesha kuzifikia kazi zako zote za umma kwenye OSF. Kwa maelezo zaidi kuhusu usimamizi wa  akaunti yako, angalia Msaada kwa Akaunti (Kiingereza)
  2. Unda Mradi
    1. Hatua zote? Wacha tuunde mradi. Miradi ni mahali pazuri pa kuhifadhi data, kushirikiana, na kuboresha mawazo yako ya utafiti! Kwa maelezo zaidi kuhusu miradi, angalia Sehemu yetu ya msaada kuanzisha Miradi (kiingereza)
  3. uanzisha Usajili mpya, Hariri Rasimu Yako ya Usajili, Wako Wasilisha Rasimu Yako ya Usajili   
    1. Usajili ni  njia ya kushirikisha wengine kwa mradi wako wa utafiti kwa uwazi na uaminifu. Usajili ni kisa rasmi cha utafiti, kuwaambia wengine mpango asili, masasisho yoyote ambayo yalihitajika, na matokeo ya mwisho. Kwa maelezo zaidi kuhusu miradi tazama Sehemu yetu ya msaadawa Usajili (kiingereza)
  4. Hifadhi ya Mradi na Upakiaji wa Faili       
    1. Baada ya kuanza utafiti wako, unahitaji mahali pa kuchakata na kushirikisha wengine data zako. Miradi ni mahali pazuri pa kufanya kazi na washirika kwenye data zako. Je, unahitaji hifadhi ya ziada kwa miradi yako? 
  5. Jinsi ya Kutayarisha Printa Yako ya Awali, Pakia Kichapo Cha Awali 
    1. Je, uko tayari kuchapisha? Wasilisha chapisho changa ambalo halija hakikiwa na watafiti wakaguzi au wachapishaji wa makala  kwenye OSF Preprints. Machapisho ya chapa za awali za makala  yaliyowasilishwa yamewekwa kwenye faharasa kwenye Google Scholar na yanaweza kukusaidia kueneza matokeo yako ya kitafiti, huku ukiyaunganisha na miradi na usajili wako wa OSF. Kwa maelezo zaidi, angalia Sehemu yetu ya msaada chapa za awali za makala (Kiingereza) Je, umeifahamu? Rudi kwenye ukurasa wetu wa mwanzo wa mwongozo wa Kuanza kutumia OSF na uone jinsi waelimishaji na watafiti kama wewe wanavyotumia OSF!

cc-zero.png

Hii Makala imeidhinishwa Chini ya leseni CC0 Kwa matumizi ya Umma wote. 


    Boakye, E., Abdullah, B., Aziz, K., Kevin, B., Kiage, B., Lisso, F., … Wesonga, R. M. (2023, May 9). Phase 1: Getting Started Help Guides (Swahili). https://doi.org/10.17605/OSF.IO/RKTHV

    Did this answer your question? Thanks for the feedback There was a problem submitting your feedback. Please try again later.